National News

TSHISEKEDI AUKACHA MKUTANO WA DHARURA

Tarehe: 29 Jan, 2025


#CONGO:Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) FĂ©lix Tshisekedi amesema kuwa hatashiriki mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulioitishwa na Rais wa Kenya, William Ruto kuhusu mgogoro wa kiusalama latika eneo la  mashariki mwa jimbo la Kivu Kaskazini mwa (DRC). 

Hata hivyo Ruto amesema kuwa amezungumza na Rais Tshisekedi pamoja na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa lengo la kujaribu kutuliza hali inayoendelea katika eneo hilo.

Hata hivyo, msemaji wa Rais Kagame amethibitisha kuwa kiongozi huyo wa Rwanda atahudhuria mkutano huo uliopangwa kufanyika leo.