#KOGOMA:Taasisi ya Kuzuia na Kupambanana Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kigoma imepokea na kuyafanyia kazi jumla ya malalamiko 70 ambapo Malalamiko 43 yanahusu Rushwa na walalamikaji walipewa ushauri namna gani na idara gani ina mamlaka ya kushughulikia malalamiko yao.
Akitoa taarifa ya ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo leo tarehe 29 Januari, 2025 katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2024 Naibu Mkuu wa (TAKUKURU) Mkoa wa Kigoma John Mgallah ameongeza kuwa katika kipindi kwenye eneo la ufutailiaji wa rasilimali za umma taasisi hiyo imefuatilia jumla ya miradi ya maendeleo 32 yenye thamani ya shilingi Bilioni kumi na moja, milioni mianne Hamsini na tatu na laki sita tisini na tisa elfu, miasita arobaini na mbili na senti sitini na saba (11,453,699,642.67)
Aidha katika ufuatiliaji huo (TAKUKURU) imebaini mapungufu madogomadogo katika miradi 31 ikiwemo kutokuwepo kwa vitabu vya kumbukumbu za stoo,kuchelewa kuanza kwa miradi na baadhi ya nyaraka za miradi kutoonekana katika majalada ya miradi .
Aidha katika sambamba na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya uchambuzi wa mifumo 2 umefanyika ili kubaini iwapo kuna mianya ya rushwa, na kisha kushauri namna ya kuiziba.
Chambuzi hizo zilikuwa za mfumo wa usajili na matumizi ya bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (ICHF) katika Wilaya ya Kakonko na mfumo wa usambazaji wa Pemberton za ruzuku kwa mwaka 2023/2024 katika Wilaya ya Kibondo.
Vilevile kupitia (TAKUKURU) Rafiki taasisi hiyo imefanikiwa kuwafuata Wananchi katika maeneo yao kwa lengo la kusikiliza kero zao, na kushirikiana nao katika kutafuta ufumbuzi wa kero hizo, ambazo zikiachwa bila kutatuliwa zinaweza kupelekea kuwepo kwa vitendo vya rushwa ambapo jumla ya kata 15 za mkoa wa Kigoma zimetembelewa na jumla ya kero 66 ziliibuliwa.