#MAREKANI:Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa taifa hilo litajiondoa kutoka kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kile alichokieleza kuwa shirika hilo limeshindwa kushughulikia kwa ufanisi janga la UVIKO-19 na majanga mengine ya afya ya kimataifa.
Vilevile Trump amesema (WHO) imeshindwa kufanya kazi kwa uhuru kutokana na ushawishi wa kisiasa usiofaa wa nchi wanachama wa shirika hilo na kudai malipo makubwa ambayo amesema yasiyo ya haki kutoka Marekani ambayo ni makubwa zaidi ikilinganishwa na kiasi kinachotolewa na nchi zingine kubwa kama China.