National News

KIJAJI ZIARANI MKOANI KIGOMA

Tarehe: 21 Jan, 2025


#HABARI: Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt. Ashatu Kijaji amefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na kupokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa.

Awali akitoa Taarifa kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Uvuvi mkoani Kigoma, Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema soko la mazao ya Samaki kwa mkoa wa kigoma limeendelea kukua na kuleta tija kwa wafanyabiashara wa bidhaa hiyo.

Aidha Rugwa amesema kwa kushirikiana na wataalam wa uvuvi, mkoa unaendelea kuhamasisha wananchi kujikita katika uvuvi wa kutumia vizimba ili kuongeza uzalishaji wa samaki pamoja na kulinda Mazingira katika Ziwa Tanganyika na kulifanya kuwa endelevu.

Kupitia ziara hiyo Mhe. Waziri Dkt. Kijaji atazindua kiwanda cha kuchakata Samaki na dagaa cha Kampuni ya LIFA sambamba na kutembelea vizimba vya kufugia samaki eneo la Katabe Beach Manispaa ya Kigoma Ujiji.