National News

WAWEKEZAJI WASIOWEKEZA ZANZIBAR WAPEWA MIEZI 3

Tarehe: 07 Jan, 2025


#ZANZIBAR:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, ametoa miezi mitatu kwa wawekezaji ambao watakuwa hawajawekeza katika sehemu mbalimbali za visiwani humo kupewa wawekezaji wengine.

Rais Samia ameyasema hayo leo tarehe 7 Januari,2025 wakati wa hafla ya ufunguzi wa hoteli ya Bawe iliyopo Visiwani Zanzibar.

"Nami nataka niungane za Rais wa Zanzibar, kwamba wale wote ambao wamepewa visiwa na hawajafanya kazi wanazunguka naa..kufanya speculation ya visiwa vyetu, basi miezi mitatu baada ya hapo mheshimiwa Rais usirudi nyuma".Ameeleza Rais Samia Suluhu Hassan.