#ARUSHA:Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo amejibu kuhusu kauli aliyoitoa mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda mbele ya Waziri wa Ujenzi Abdalla Ulega akimtaka kuwa na utaratibu wa kuhudhuria vikao vya Halmashauri.
Akieleza kuhusiana na kauli hiyo Gambo amesema kuwa mwenye wajibu wa kutoa taarifa na rekodi kuhusu kuhudhuria vikao kwa mujibu wa seheria ni Bunge la Jamhuri ya muungao wa Tanzania.
Katika hatua nyingine amesema kuwa yeye siyo mfanyakazi wa serikali bali ni Mwakilishi wa Wananchi na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.