#DODOMA:Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) CPA Amos Makalla, amesema kuwa Mkutano Mkuu wa Chama hicho utafanyika tarehe 18-19 Januari,2025.
Makalla ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 7 Januari,2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho Mkoani Dodoma na kubainisha kuwa, kupitia mkutano huo pia kutafanyika uchaguzi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho kwa Tanzania Bara ambayo ilikuwa inaongozwa Abdulrahman Kinana aliyejiuzulu.
Pia kupitia Mkutano huo watapokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho, kutoka serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.