National News

DKT.BITEKO ASISITIZA MAADILI UNUNUZI NA UGAVI

Tarehe: 17 Dec, 2024


#ARUSHA:Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko amewataka Wataalam wa Ununuzi na Ugavi kuendelea kusimamia maadili ili kuhakikisha kila mwanataaluma wa kada hiyo anakuwa na viwango vya juu vya maadili.

Dkt. Biteko amezungumza hayo kwenye kongamano la 15 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi leo 17 Disemba,2024 lililofanyika kwenye kituo cha cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC Jijini Arusha, ambapo ameeleza anaamini kuwa wataendelea kusimamia maadili kwa kuzingatia mitaala iliyopo ili kuhakikisha kuwa kila mtaalam wa Ununuzi na Ugavi anayekiuka maadili ya kazi hiyo anachukuliwa hatua bila huruma.

"Nimeambiwa hapa kuwa, katika mwaka tu huu uliopita mlikuwa na mashauri 32 ya Wanataaluma wenzenu ambao wamefanya vitendo ambavyo haviendani na Taaluma yenu, nimefurahi kuwa 14 kati yao uamuzi umetoka na wamepewa adhabu".Alieza Dkt. Dkt. Biteko

"Mimi sifurahii watu kupewa adhabu, lakini at least kuonesha kuwa hakuna anayeweza kufanya kosa akabiki akifurahia na kuifanya Taaluma yote kuonekana haina maana kumbe ni kwasababu ya mtu mmoja".Alisisitiza Dkt.Biteko.

Katika hatua nyingine Dkt.Biteko amempongeza mkuu wa mkoa wa Arusha Paul  Makonda kutokana na nmna anavyoendana na Wananchi wa  mkoa huo huku akisema kuwa kama kungekuwa na like kwenye maneno yake angegonga like.

"Unajua kuna wakati fulani huwa huwa mimi najiuliza sana, kwamba wewe umepewa mafasi mahali fulani ili uwahudumie watu,basi unachukua muda mwingi kubishana rasilimali kidogo zinazowahusu watu haziwafikii na bado tu unasimama unanyoosha mkono kwenye msiba kujitambulisha kwa cheo chako...yaani huna hata hiyo aibu" alidokeza Dkt. Biteko.