TANZANIA YASHIRIKI KAMBI UTAFITI VIPAJI KIDIJITALI
Tarehe: 05 Dec, 2024
#HABARI:Wanafunzi wa Tanzania wameshiriki Kambi ya Utafiti wa Vipaji vya Kidigitali ya Huawei Kusini mwa Jangwa la Sahara nchini China (Leap Digital Study).
Kwa mara nyingine tena Shenzhen, Huawei kwa mara imedhihirisha dhamira yake ya kuwawezesha vijana wenye vipaji katika nyanja za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) kwa kuandaa Kambi ya Utafiti wa Vipaji vya Kidigitali ya Huawei kutoka katika nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (LEAP) liliofanyika kuanzia Novemba 18 -22 Novemba, 2024 nchini China .
Mpango huo wa kidijiti umedhamiria kutoa maarifa ya uongozi, na kutoa uwezekano wa fursa za kuajiajiri ukilenga zaidi kukuza stadi za juu katika tasnia ya kidijitali na kukuza uvumbuzi miongoni mwa vipaji vya vijana kutoka kanda ya Afrika.
Kambi hiyo, iliyofanyika katika makao makuu ya kimataifa ya Huawei huko Shenzhen, China ni sehemu ya dhamira pana ya Huawei ya kuendeleza wafanyakazi wenye ujuzi katika anga za kidijitali kote barani Afrika, ambayo ilileta pamoja wanafunzi wenye vipaji vya kipekee kutoka nchi 17 za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa ni pamoja na Tanzania, Nigeria, Afrika Kusini,Mauritius, Kenya, na zaidi
Pia kambi hiyo ya utafiti iligusa ajenda muhimu za kidijitali ikijumuisha kozi za (ICT) kuhusu teknolojia ya kisasa kama vile Akili Mnemba (AI), Mawasiliano ya mtandao wa 5G, nguvu za kidijitali, teknolojia za masafa pamoja na kongamano la uongozi.
Tukio hilo la wiki moja lilifikia kilele kwa kuandaliwa shindano la Tech4 Good, ambapo washiriki kutoka nchi tofauti waliunda timu ili kuja na majawabu kupitia teknolojia yanayojibu changamoto za kijamii.
Tanzania pia iliwakilishwa na Wanafunzi 10 bora kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) ambapo Huawei ilitoa ufadhili kamili kwa safari za ndege za kwenfa na kurudi, malazi na mafunzo kwa washiriki wote, ili kuhakikisha kwamba umakini wao unabaki kwenye kujifunza .
Kambi hiyo ya Utafiti wa Vipaji vya Kidijitali ya (LEAP), ilizinduliwa na Huawei katika nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara mnamo mwaka 2022, ikiwa ni sehemu ya mpango wake mpana wa kukuza wafanyakazi wenye ujuzi katika anga za kidijitali kote barani Afrika.
Hata hivyo Huawei inatazamiwa kuinua dhamira yake ya kuendeleza vipaji vya kidijitali katika Afrika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kutoa mafunzo kwa vijana 150,000 kupitia mpango wake wa kukuza ujuzi wa kidijitali wa (LEAP) katika miaka mitatu ijayo huku mpango huo ukiwa ni sehemu ya mkakati mpana wa Huawei wa kuwekeza katika rasilimali za kimataifa zinazolenga kukidhi mahitaji mahususi ya vipaji vya kidijitali vya jumuiya za wenyeji.
Mpango wa (LEAP) umeundwa ili kuziba pengo la ujuzi wa kidijitali katika nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kutoa mafunzo na nyenzo za kina. Ikilenga katika kukuza uongozi wa kidijitali, kujenga wafanyakazi wenye ujuzi wa (ICT) kuunda kundi la vijana wenye vipaji vya kidijitali, na kuimarisha ujuzi wa kidijitali miongoni mwa wananchi.
Kwa kufanya hivyo, Huawei inalenga kuleta athari kubwa kwenye uwezo wa kidijitali na matarajio ya siku za usoni za nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.