National News

MABALOZI WATAKIWA KUITANGAZA ZANZIBAR KIMATAIFA

Tarehe: 05 Sep, 2023


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka Waheshimiwa Mabalozi walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali Duniani kuitangaza Zanzibar katika fursa za sekta ya utalii, uwekezaji , ufadhili wa masomo, misaada ya teknolojia, mikopo yenye masharti nafuu, kuitangaza sera ya uchumi wa buluu na fursa za kibiashara na soko la bidhaa za ndani  za viungo likiwemo zao mama la karafuu.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo tarehe 05 Septemba alipokutana na  Waheshimiwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali akiwemo Mhe. Joseph E.Sokoine, Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe.Fatma M.Rajab , Balozi wa Tanzania nchini Oman , Mhe.Naimi S.H.Aziz Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe.Ali Mwadini , Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe.Ceasar Waitara , Balozi wa Tanzania nchini Namibia waliofika Ikulu Zanzibar kwa kujitambulisha na kumuaga.

Chanzo:Ikulu, Zanzibar.