National News

14 WANUSURIKA KIFO AJALI YA TRENI

Tarehe: 10 Nov, 2024


#HABARI:Watu 14 wamenusurika kifo katika ajali iliyotokea alfajiri ya kuamkia leo katika makutano ya reli na barabara kati ya Malagarasi na Nguruka mkoani Kigoma, baada ya basi la abiria kampuni ya Classic kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Kigoma kwenda Tabora.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Shirika la Reli Tanzania (TRC) Fredy Mwanjala imesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 4:20 usiku, huku chanzo kikiwa ni dereva wa basi kuendesha bila kuzingatia sheria.

"Äjali imesababisha mabehewa matano kati ya 30 kuanguka, abiria wapatao 14 kati yao wanawake nane (8) na wanaume sita (6) waliokuwa wakisafiri na basi hilo wamepata majeraha madogo na hakuna abiria aliyepoteza maisha", imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.