National News

SERIKALI ILITOA MSAMAHA 25% USHURU WA FORODHA

Tarehe: 06 Nov, 2024


#NISHATI:Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema kupitia Bajeti Kuu Serikali ya mwaka (2023/24) Serikali ilitoa msamaha wa kodi ya ushuru wa forodha (customs duty) asilimia 25% kwa injini za Magari yanayotumia gesi asilia yanapoingizwa nchini. 

Kapinga ameyasema hayo leo Novemba 06, 2024 Bungeni Jijini Dodoma  wakati akijibu swali la la Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Tendega aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali kupunguza baadhi ya kodi kwenye magari yanayotumia mfumo wa gesi ili Watanzania wengi waweze kuyaagiza.

 "Tuaendelea na hatua mbalimbali za kuhamasisha sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye viwanda vinavyo tengeneza vipuri vinavyotumika katika kufunga mfumo wa matumizi ya gesi asilia kwenye magari na mitambo hapa nchini". Amesema  Kapinga 

Kuhusiana na usambazaji  wa umeme Vijijini, Vitongojini na kwenye mitaa  Kapinga  amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati imejidhatiti kuhakikisha maeneo yote nchini yanapata huduma ya umeme.

Aidha, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Ester Matiko aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali katika kubadili magari yanayotumia mfumo wa Dizeli kwenda kwenye gesi, Kapinga amesema  Serikali inaendelea kuwekeza kwenye vituo zaidi ili kuhakikisha pia na magari yanayotumia Dizeli yanaanza kutumia mfumo wa gesi.

Ameongeza kuwa kutokana na utofauti uliopo kati ya magari yanayotumia petroli na Dizeli ilikuwa ni rahisi kwa Serikali kuanza na magari ya petroli kabla ya yanayotumia Dizeli.