National News

MZAVA ASISISTIZA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST

Tarehe: 16 Sep, 2024


#KIGOMA:Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 Ndg.Godfrey Eliakimu Mzawa amesisitiza kuhusu matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma NeST katika kutangaza zabuni mbalimbali zinazotolewa na Serikali ili kuongeza uwazi na uwajibikaji, udhibiti mzuri katika manunuzi hayo, kuondoa manung'uniko na kuongeza kuwa kumekuwa na manung'uniko ya kukisia kuwa kuna watu wanapendelewa katika miradi hiyo hivyo kupitia mfumo huo serikali inaamini kuwa hakutakuwa na changamoto hiyo.

Mzava ameyasema hayo leo tarehe 16 Septemba,2024 wakati wa mbio za Mwenge katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma kwaajili ya kukagua,kuzindua na kuweka jiwe la msingi baada ya kusomewa ripoti ya mradi wa barabara ya Stanley katika manispaa hiyo kuukagua na kuuzindua ambao umezingatia matumizi ya mfumo huo na kuongeza kuwa utaratibu huo unamsaidia kila aneyeomba  zabuni kuweza kuona taarifa zake ikiwa ni pamoja na kujua vigezo vya kupata zabuni husika.

"Maelekezo ya serikali ni kwamba katika miradi yote ya umma kama inatumia fedha yoyote kutoka serikali kuu,Wahisani,Wadau wa maendeleo, fedha ya mapato ya ndani zabuni zake kwenye kuwapata kama ni Wakandarasi, mafundi,kama ni kupata huduma ama vifaa manunuzi yote ni kwenye mfumo.Kwahiyo taasisi nunuzi zote ndani ya Manispaa ya Kigoma Ujiji zinaendelea kusisitiziwa matumizi sahihi ya mfumo wa NeST, na huo ndiyo mfumo wa serikali  ambao unakwenda na mapinduzi haya ya Sayansi na Teknolojia, sasa hadi kwenye mifumo ya uendeshaji wa shughuli za kiserikali lazima twende huko".Amesisitiza Ndg.Mzava.

Aidha miradi mbalimbali imezinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi ikiwemo  Mradi wa uboreshaji wa Chanzo cha Maji Kibirizi  ambao unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya Maji safi kwa wakazi wa kijiji cha Kalalangabo, wilayani Kigoma ambapo taarifa ya mradi huo iliyosomwa na Meneja wa Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA), Yasinta Jovin, imesema kuwa mradi huo umegharimu shilingi milioni 160. 
Mradi huo umehusisha ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita elfu 78, uwekaji wa pampu mpya, na mtandao wa mabomba wenye urefu wa kilometa 1.1.

Mradi huo ni maboresho ya chanzo cha zamani cha maji na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakazi 2,000 wa kijiji cha Kalalangabo, kata ya Ziwani ambapo awali hao walikuwa wakilazimika kutumia maji yaliyotokana na chemchem na Ziwa Tanganyika.@kigomaujiji @kigomars