HESLB YAWAHIMIZA WANUFAIKA WENYE KIPATO KUREJESHA MIKOPO
Tarehe: 13 Sep, 2024
#HABARI:Bodi ya mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imewahimiza wanufaika wenye kipato kuhakikisha wanarudisha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha wanufaika wengine kupata mikopo hiyo.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mtendaji wa (HESLB) Dkt. Bill Kiwia wakati wa hafla kubadilishana hati za ushirikiano kati ya bodi ya mikopo na mamlaka ya mapato (TRA) lengo likiwa ni kuwafikia wanufaika wengi zaidi.
Kwa upande wake kamishna mkuu wa (TRA) Yusuph Mwenda amebainiaha kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na bodi kwa kutoa taarifa zote za msingi za wanufaika wenye shughuli za kiuchumi.