ANDENGENYE AWAJULIA HALI WATUMISHI WA AFYA WALIOPATA AJALI
Tarehe: 11 Sep, 2024
#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye leo Septemba 11, 2024 amewatembelea watumishi wa Idara ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni kufuatia ajali waliyoipata katika kijiji cha Nyamoli kilichopo wilayani humo Septemba 10, 2024 wakitoka kutekeleza majukumu yao ya kiutumishi.
Akiwa hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa amemtembelea Bi. Flora Ezebius, Mratibu wa Huduma ya Mama, Baba na Mtoto Halmashauri ya Kigoma ambaye amevunjika mkono wa kulia sambamba na Julius Mbise, Dreva wa Idara ya Afya katika Halmashauri hiyo ambaye amevunjika Mguu wa Kushoto.
Mhe. Andengenye amewatakia heri kiafya ili waweze kupona haraka huku akiwasisitiza wataalam wanaowahudumia kuendelea kuwapa huduma kwa ukaribu ili waweze kupona na kurejea katika majukumu yao ya kila Siku ya kuwahudumia watanzania.
Aidha watumishi wengine wawili waliokuwemo kwenye ajali hiyo wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kuendelea na majukumu yao.