National News

DC MTWARA AFUTWA KAZI

Tarehe: 27 Aug, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifunga mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Wa Mikoa katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani leo ametangaza kumfuta kazi Mkuu wa wilaya ya Mtwara kwa kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.

“Siwezi kustahamili kadi za chama zinarudishwa, Mkuu wa wilaya yupo, DED yupo ,Namtimua leo ,kadi za chama zinarudishwa watu wanashida anaulizwa anasema  ,ooh unajua kule wengi wapinzani. So what? Si watanzania wale, hawahahitaji kitu? Sina imani na Mkuu wa wilaya anayesababisha kadi zirudishwe"- Rais Samia.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania5
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania