#KIGOMA:Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa lengo la kujipatia fedha kinyume na sheria kwa kuwatapeli wazazi wao ili wawatumie kiasi cha pesa kwaajili ya kuachiwa huru.
Akizungumzia tukio hilo mbele ya waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Kigoma SACP Filemon Makungu amesema kuwa Mei 14 mwaka huu mtu aliyefahamika kwa jina la Ramadhan Shaban mkazi wa Kichwele manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma alidai kutekwa akiwa anatoka kwa bibi yake na kutoa taarifa kutumwa kiasi cha shilingi Milioni 2,500,000/= ndipo aachiwe huru.
"Alidai kutekwa akiwa anatoka kwa bibi yake baada ya kujificha na kutoa taarifa ya uongo kwa wazazi akiwashinikiza kutoa kiasi cha shilingi milioni 2,500,000/= ndipo mtoto wao aachiwe huru,taarifa hiyo aliyeripotiwa kutoa taarifa kituo cha polisi wazazi walikuja kuripoti kuwa kijana wao amepotea wakati akitoka kwa bibi yao,tukafungua jalada la uchunguzi na baadaye akaja kupatikana tarehe 25 mwezi wa tano 2024 na akafikishwa kituo cha polisi" Amesema SACP Makungu.
Kamanda Makungu ameongeza kuwa baada ya taarifa za kupotea kwake kuripotiwa kituo cha polisi uchunguzi ulianza maramoja na kubaini ukweli kuhusiana na tukio hilo ambapo Mei 25 mwaka huu majira ya saa 4:00 usiku mtuhumiwa huyo alifikishwa kituo cha polisi eneo la Msimba maeneo ya Dampo baada ya kutuma kiasi cha pesa walichotaka kitumwe.
Aidha kamanda huyo amewataja watu hao wawili walioshirikiana na mtuhumiwa huyo kugawana kiasi hicho cha pesa kuwa ni Kassim Kibona na Ramadhan waliotoa taarifa za uongo kwenye tuko hilo.