Sports

DABO APEWA 'THANK YOU' AZAM

Tarehe: 03 Sep, 2024


#MICHEZO: Bodi ya wakurugenzi ya Azam FC na kocha Youssouph Dabo wamefikia makubaliano ya pande mbili ya kutoendelea kufanya kazi pamoja kuanzia leo Septemba 3, 2024.

Dabo aliyehudumu Azam FC kwa kipindi cha mwaka mmoja anondoka na wasaidizi wake wa benchi la ufundi aliokuja nao.

Bodi ya Azam FC ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya, kipindi hiki programu za timu zitakuwa chini ya makocha wa timu za vijana.