National News

RAIS SAMIA KUHUTUBIA MKUTANO WA FOCAC CHINA

Tarehe: 03 Sep, 2024


#HABARI:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa jukwaa la viongozi wakuu wa nchi za Afrika  na China  mkutano unaotarajiwa kuaanza tarehe 4-6 Agosti,2024
Katika ziara  hiyo nchini China .

Aidha Rais Samia atashiriki Mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo pia anatarajia kuhutubia  ufunguzi wa mkutano  huo.

Katika hatua nyingine atafanya mazungumzo na Rais wa  China, Xi Jinping na kushuhudia uwekaji saini wa Hati za makubaliano ya uboreshaji wa Reli ya (TAZARA) ambapo pia atakutana na makampuni na wawekezaji kutoka China ili kuhamasisha uwekezaji zaidi nchini Tanzania.