Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC) imemtangaza Emmerson Mnangagwa kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais kwa kura 2,350,711 sawa na 53% ya Kura ambapo Kiongozi huyo aliingia Madarakani tangu mwaka 2017.
Aidha Tume hiyo ya uchaguzi imesema Mpinzani Mkuu wa Mnangagwa katika kinyang'anyiro hicho, Nelson Chamisa ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Citizens's Coalition for Change (CCC), alipata kura 1,906,734 sawa na 44% ya Kura, japo kuwa Chamisa amekataa Matokeo hayo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo, hata hivyo Agosti 26, mwaka huu Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU OEM) walidai kuwa Uchaguzi huo haukuwa Huru na Haki.