#HABARI:Madiwani wanaounda kamati ya kudhibiti UKIMWI wakiogozwa na naibu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Momba mkoa wa Songwe mheshimiwa Njanvwa Jackson Sihame wamefanya ziara ya mafunzo katika halmashauri ya manispaa ya Temeke na kupokelewa na mwenyeji naibu meya mheshimiwa Anorld Peter, madiwani wanaounda kamati hiyo, kaimu mkurugenzi wakili Faraja Nakua na wataalam wa idara ya Afya wakingozwa na mganga mkuu Jonas Lulandala.
"Tumekuja kujifunza namna kamati ya kudhibiti UKIMWI manispaa ya Temeke inapanga na kufanikisha udhibiti na kuelimisha zaidi juu ya maambukizi ya UKIMWI.Tumejifunza kuwa, kamati imefanya shughuli kuwa nyepesi kwa kushirikiana kikamilifu na wataalam wa ngazi zote na jamii yenyewe" Alieleza Sihame.
Aidha madiwani hao wametembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke (TRRH) na kujionea huduma kwa waathirika wa virusi vya UKIMWI na madawa ya kulevya zinavyotolewa pamoja na mikakati mbalimbali ya elimu na udhibiti inayotolewa na hospitali hiyo chini ya uongozi wa daktari Joseph Kimaro.
Manispaa ya Temeke imeendelea kuwa mwenyeji kwa halmashauri mbalimbali kwa kushiriki katika mafunzo na kubadilishana utaalam ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia Wananchi.