#KIGOMA:Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi Nchini kuwasimamia Wahudumu wa afya ili kuhakikisha wanatoa Matibabu kwa Wananchi yaliyo bora ikiwa ni pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto zao pamoja na Wanachi.
Kiongozi huyo ametoa maelekezo hayo Agosti 12, 2024 baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi unaoendelea ili kuhakikisha inakidhi vigezo na viwango vya Hospitali za Wilaya ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali za kibingwa.
Aidha Waziri Mchengerwa amemuagiza Mkurugenzi wa afya OR- TAMISEMI kutoa kiasi cha fedha za Kitanzian Bilioni mbili (Tsh 2, 000, 000, 000/=) kwa ajili ya kuongeza majengo kufikia kumi na sita (16) katika Hospitali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Awali akitoa taarifa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Dr. Hashim Mvogogo amesema awali Serikali Kuu ilitoa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Majengo matano (05) kiasi cha fedha za Kitanzania Billion Moja na Million Mia tatu (Tsh 1, 300, 000, 000/=) kwa ajili ya Ujenzi waJengo la Wagonjwa wa nje (OPD), Maabara, Jengo la Wazazi (Maternity Complex), Jengo la mionzi, na jengo la stoo ya dawa.
Aidha kiongozi huyo amefanya ziara ya kutembelea Ujenzi wa barabara ya Bangwe - Ujiji unaoendelea yenye urefu wa Km 7.01 kupitia mradi wa uboreshaji wa Miji Kimkakati (TACTICS) ambapo amesema mradi huo uko chini kwa utekelezaji ambapo uko asilimia 18% Badala ya kuwa asilimia Sitini (60%).
Kiongozi huyo ametoa miezi sita kuanzia sasa kuhakikisha Mkandarasi anakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha Lami, Mitalo na Ufungaji wa taa.