#AFYA:Imeelezwa kwamba Kumekuwa na ongezeko kubwa la magojwa yasiyoambukiza ambapo kwa kwa mwaka 2022/23 hospitali ya rufaa ya Temeke ilihudumia wagonjwa wapatao 9566 huku mwaka 2023/24 wakifikia wagonjwa 11,175 sawa na Ongezeko la asilimia 14.4
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sixtus Mapunda wakati alimpomuwakilisha waziri wa afya Ummy Mwalimu kwenye hafla ya makabidhiano ya jengo la kutolea huduma za kusafisha damu katika hospitali ya rufaa ya Temeke ambapo pia amewataka wahudumu wa afya Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza huku jamii ikitakiwa kuzingatia mtindo bora wa maisha
Akitoa taarifa ya hospitali hiyo mganga mkuu Dkt Joseph Kimaro amesema mwaka 2023/24 hospitali ilipokea takribani wagonjwa 412 waliohitaji huduma za usafishaji damu ambao walipatiwa rufaa hivyo kuanzishwa kwa huduma hiyo kutasaidia kusogeza huduma hizo karibu na wananchi.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa bandari ya dar es salaam Abeid Galus amesema TPA itaendelea kushiriki katika miradi mbalimbali ya kijamii ambapo kwa sasa imetoa Shilingi milioni 251.26 kwa ajili ya maboresho ya jengo hilo pamoja na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 10.