National News

VIJANA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA BIASHARA YA FIGO

Tarehe: 22 Jul, 2023


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania hususani vijana kujiepusha na kutoa figo zao kwaajili ya kufanya biashara ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza.

Akiwa ziarani mkoani Ruvuma Dkt. Mpango pia amezindua Jengo la kutolea huduma ya usafishaji figo lililopo katika hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph - Peramiho ambapo amesema tabia ya kuuza figo inaweza kuhatarisha Maisha ya mwanadamu hususani pale figo iliobaki inaposhindwa kufanya kazi.