National News

BUNDI, NGEDELE WASABABISHA HITILAFU SGR

Tarehe: 31 Jul, 2024


#HABARI: Shirika la Reli Tanzania (TRC), limeomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili usiku wa jana July 30, 2024.

Taarifa ya leo Julai 31, 2024 ya Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano - TRC, Jamila Mbarouck imebainisha kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system)”

“Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku”

“Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku, Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu” — imesema taarifa hiyo.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab