National News

JKCI YATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA

Tarehe: 29 Jul, 2024


#HABARI:Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kiketwe (JKCI)- Dar Group imetekeleza agizo la  Rais wa Jamhuri wa Muungaano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kila mkoa kuwa na Plant ya Oksijeni ambapo wamezindua mitambo ya kuzalisha Oksijeni ulioghrimu shilingi Milioni 526,604,116.

Mtambo huo unatumia umeme wa KVA 60 na kuzalisha hewa ya Oksijeni yenye ujazo wa Milmita Skwea 21 kwa saa yenye kasi ya Mita Skwea 5 kwa saa wakati wa kujaza kwenye mtungi.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa mitambo hiyo, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunhe wa Ilala, Mussa Azzan Zungu aliiomba Taasisi hiyo kuweka gharama ndogo za matibabu kupitia mtambo huo ili kusaidia mfuko wa NHIF kuweza kutokulipa gharama nyingi kwa wagonjwa.

Pia alisema  kwa sasa vipo vyumba vya (ICU) vinavyochaji pesa nyingi bila kuweka gharama za dawa ambapo wakiweka na dawa gharama zinakua juu sana hivyo aliwataka watibabu kuwa sehemu ya kuchangia ghamara ili na wao waweze kupata huduma safi na salama na kupunguza makali ya mfuko wa NHIF .

“Sasahivi kuna vyumba vya ICU vinachaji mpaka laki tano bila kuweka gharama za dawa , mungu ametuoa oksijeni tunaivuta bure, ila tukipata matatizo ya kiafya lazima uje utibiwe na mtambo huu hivyo watibabu muwe sehemu ya kuchangia gharama ili na wao waweze kupata huduma safi na salama na kupunguza makali ya mfuko wa NHIF”Ameeleza 

Aidha Zungu amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kufanya uwekesaji  kwenye sekta ya  afya, na kuwataka (JKCI) kuhakikisha huduma hizo ambazo Rais Samia ameendelea kuziwekea mkazo zinawafikia watanzania wote.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete  Dkt. Delilah Kimambo alisema Mtambo huo utasaidia  kupunguza gharama za uendeshaji kwa asilimia zaidi ya 3.7 kwa mwaka wa kwanza na  hivyo kuleta urahisi wa itoaji huduma kwa wagonjwa wao kwa haraka 

Pia amesema  kuwa Mtambo huo utaongeza  ufanisi wa huduma na kasi ya hospitali hiyo na  kufikia safari ya viwango vya kimataifa ambapo uzalishaji ukiongezeka wataendelea  kutoa huduma hiyo katika hospitali zinazowazunguka. 

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya uzazi mama na mtoto, Dkt. Ahmad Makuwani alisema Wizara imeipongeza timu ya JKCI kwa kubadili muonekano wa JKCI, kutunza ajira  na kuondoa rufaa za moyo kwenda nje ya nchi, lakini pia kutibu watanzania na wananchi kutoka nchi za nje kwa magonjwa hayo ya moyo.