#HABARI:Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri amesema katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2023/24 kituo cha uwekezaji kilisajili miradi 707 yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni 6.5 na zinazotarajiwa kuleta ajira ya zaidi laki mbili na Ishirini na Tano (225,000), na kumekuwepo na ongezeko la zaidi ya asilimia 400 kutoka ajira takribani elfu hamsini (50,000).
Teri amebainisha hayo Leo Julai 25, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa wawekezaji wa ndani, wenye lengo la kusikiliza changamoto zao na kuwafikishia mikakati ya serikali katika uwekezaji nchini.
Amesema kuwa Sekta zinazoongoza katika uwekezaji nchini ni Tano ambazo ni Sekta ya Viwanda, Uchukuzi, Majengo ya kibiashara, Utalii na Kilimo, huku mitaji ikiwa na ongezeko la asilimia ishirini na moja na miradi 360 ilisajiliwa mwaka wa fedha uliopita 2022/23.
"Tumejumuika na TRA, Brela, Nemc na Idara ya kazi na uhamiaji na maeneo yanayotoa huduma Kwa wawekezaji ili kutoa majibu ya changamoto wanazokutana nazo.
"Kubwa ni ongezeko la wawekezaji wa ndani, watanzania waliojisajili miradi yao mwaka Jana ilikuwa ni asilimia 38 ya uwekezaji tuliyosajili, watanzania walioshirikiana na wageni kama wabia ilikuwa asilimia 20, na kufanya kuwa jumla ya asilimia 58 ya miradi kuwa na mikono ya watanzania, na ndio lengo l Rais Samia wakati anabadiisha Sheria ya uwekezaji.
Kwa upande wake, Muwekezaji ambaye ni Mmiliki Kiwanda Cha Kahawa Mumunyifu, Amir Hamza ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kazi kubwa ya kuweka mazingira mazuri Kwa wawekezaji pamoja na kubadilisha Sheria ya uwekezaji.