National News

FRANK SHANGALI MENEJA MPYA USIMAMIZI IGT

Tarehe: 20 Jul, 2024


#UTEUZI:Kamishna mkuu wa Usimamizi wa Bima nchini Tanzania Dkt. Baghayo Saquare, amemteua Bwana Frank  Fred Shangali  kuwa memneja Usimamizi wa kampuni ya Bima ya Insurance Group of Tanzania (IGT) na huo umeanza rasmi tarehe 19 Julai 2024.

Kupitia barua iliyotolewa na Mamlaka ya usimamizi wa bima nchini (TIRA), uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa sheria ya Bima sura 394, kifungu cha 165 (1)(iv) ambacho kinampa mamlaka kamishna kuteua meneja wa muda ambaye atakuwa msimamizi wa kampuni ili kuimarisha utendaji wa kampuni husika.

Kabla ya Uteuzi huo Bw. Fank Shangali amekua meneja katika vitengo mbalimbali ndani ya mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa msaidizi katika  idara ya  na ukaguzi wa makampuni ya Bima, na kuhudumu kama meneja wa kanda ya Mashariki. 

Pamoja na  uteuzi huu Frank  ni Meneja wa kanda ya kati wa Mamlaka ya Bima nchini.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab