National News

ASKOFU MALASUSA MKUU MPYA KKKT

Tarehe: 25 Aug, 2023


Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uliokuwa ukifanyika mkoani Arusha,  umemchagua Askofu Alex Malasusa kuwa Mkuu Mteule wa kanisa hilo akichukua nafasi ya Askofu Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake.

Askofu Malasula amechaguliwa kwa kura za ndio 167 ambazo ni sawa na asilimia 69.3 kati ya kura 241 zilizopigwa.

Askofu Malasusa anarejea tena kwenye nafasi hiyo ambayo aliwahi kuishika kwa muda wa miaka 8 kuanzia mwaka  2007 hadi 2015.

Wagombea wengine katika nafasi hiyo walikuwa ni Askofu Abednego Kesho Mshahara wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi na Askofu George Mark Fihavango wa Dayosisi ya Kusini.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab