HABARI: Kufuatia kauli yake aliyoitoa akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko la Kashai, mjini Bukoba Julai 15, 2025 ambayo imezua mjadala mtandaoni, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewaomba radhi Wananchi na wapenda demokrasia Nchini.
Akiongea leo July 17,2024 Nape amesema “Kama nilivyosema kwenye tweet yangu huu ni utani sasa nadhani umekuwa mjadala mrefu this time kwasababu tunaelekea kwenye uchaguzi lakini niseme kama Kiongozi, Mtu mzima nadhani nawajibika kuwapa pole na kuomba radhi”
“Mimi ni Muumini wa uchaguzi huru na wa haki na kuwapa fursa Wapiga kura wao kuchagua Kiongozi wanayemtaka” - Amesema Nape.
Waziri Nape akiwa Bukoba Juzi katika kauli yake alinukuliwa akisema "Wengine wasubiri kwani wakisubiri kuna shida!? mwacheni aendelee na Mimi nitamsaidia ashinde na kwasababu Mimi mjanja wa uchaguzi nitamfundisha”
“Unajua matokeo ya kura sio lazima yawe yale ya kwenye box inategemea nani anahesabu na kutangaza na kuna mbinu nyingi kuna halali, nusu halali na haramu, na zote zinaweza kutumika ilimradi tu ukishamaliza unamwambia Mungu nisamehe” - Kauli ya Waziri Nape akiwa Bukoba.