National News

HAKUNA MGAO WA UMEME TENA NCHINI,

Tarehe: 09 Jun, 2024


#UMEME:Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, kwa sasa nchi ina umeme wa kutosha  kuwawezesha Watanzania kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Juni 9, 2024 wakati alipoungana na Waumini wa Kanisa la AIC Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kwenye ibada ya jumapili.

"Nashukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia ameweka mipango madhubuti kwenye sekta yetu ya nishati ambayo sasa imepelekea tuwe na umeme wa kutosha na hatuna mgawo wa umeme." Amesema Dkt. Biteko

Ameongeza kuwa,  miezi michache iliyopita, tatizo la mgawo wa umeme  lilikuwa likimkosesha amani, lakini  kwa juhudi za viongozi Wakuu wa Serikali, Wizara na TANESCO limefikia tamati. 
 
Kutokana na uwepo wa umeme mwingi wa  kutosha, Dkt. Biteko amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kwamba Serikali inaendelea kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.