National News

CCM YAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI ZOEZI UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

Tarehe: 06 Jun, 2024


#UHAMASISHAJI: Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma  Mkoani Kigoma kimefanya vikao katika vituo vinne katika kata zote za Wilaya ya Kigoma katika Vijii. 

Lengo la vikao hivyo ni kuhamasisha wanannchi kujitokeza kwa wingi katika uandikishaji wa daftari la mpiga huku viongozi wakiagizwa kuhamasisha zoezi hilo katika maeneo yao. 

Ikumbukwe kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la kidumu la mpiga kura kitaifa linatarajiwa kuzinduliwa tarehe 1Julai,2024 katika mkoa wa Kigoma ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ambapo mkoani hapa zoezi hilo litaanza tarehe 1-7 Julai, 2024.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab