National News

WASIMAMIZI MAGATI KIGOMA WAWAKUMBUSHWA KUFUATA UTARATIBU

Tarehe: 05 Jun, 2024


#KIGOMA:Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA) Ndugu Poas Kilangi amewataka wasimamizi wa Magati kufuata taratibu za uendeshaji pamoja na mikataba walioyoingia pamoja na KUWASA ambayo inawataka kufanya malipo ya fedha wanazokusanya kutoka kwa wananchi kwa wakati ili kuepuka madeni ambayo yanawezasababisha kusitishwa kwa huduma

Kilangi ameyasema hayo leo tarehe 5 Juni,2024  alipofanya  kikao na Wasimamizi wa Magati pamoja na Wenyeviti wa Vitongoji wa Kijiji cha Kalalangabo Halmashauri ya Kigoma.

Vilevile katika kikao hicho Kilangi amewataka wasimamizi wa Magati kufuata taratibu za uendeshaji pamoja na mikataba walioyoingia pamoja na KUWASA ambayo inawataka kufanya malipo ya fedha wanazokusanya kutoka kwa wananchi kwa wakati ili kuepuka madeni ambayo yanawezasababisha kusitishwa kwa huduma.

Sambamba na hayo  amewahakikishia wasimamizi na wenyeviti wa vitongoji kuweka ratiba nzuri ya upatikanaji wa maji wakati maboreshi ya chanzo yakiendelea ili kutimiza mahitaji ya wananchi.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab