National News

BENKI YA DUNIA YAIPA KONGOLE TANZANIA

Tarehe: 04 Jun, 2024


#PONGEZI: Tanzania imepongezwa na Benki ya Dunia kwa kuwa miongoni mwa nchi inayoongoza kusambaza Nishati ya Umeme kwa wananchi wake

Akizungumza leo Juni 4, 2024 ofisini kwake jijini Dodoma, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameishukuru Benki ya Dunia kwa pongezi hizo na kusema kuwa Benki hiyo ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini na kuwa wamekuwa na ajenda ya kushirikiana katika miradi ya nishati.

“Tumefurahi kusikia nchi yetu imepiga hatua na tumejipanga kuendeleza miradi mingine ya nishati ili kuhakikisha kuna utoshelevu wa Nishati hiyo nchini", amesema Dkt. Biteko.

Dkt.Biteko ameongeza kuwa wataendelea kushirikiana na Benki ya Dunia na na kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza kila fedha tunayopata lazima iwe na thamani kwa wananchi. Wizara pamoja na Shirika letu la umeme TANESCO limepongezwa kwa kushughulikia vizuri suala la nishati nchini,huku akisisitiza kuwa  ni lazima kuangalia mbali zaidi si tu kuridhika na hali iliyopo kwa sasa. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete amesema kuwa Benki hiyo inatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na mfumo mzuri wa kusambaza nishati kwa Watanzania.

“Hapa Afrika, Tanzania ni mfano mzuri katika usambazaji wa Nishati ya Umeme kwa wananchi. Tumejipanga kuwa na mazungumzo zaidi na kuona namna bora zaidi ya kusaidia katika masuala ya nishati safi ya kupikia kwa kufadhili na  kuhusisha sekta binafsi kwa kuangalia fursa zilizopo”, amesema Belete.

Vilevile Bw. Belete amesema kuwa Benki hiyo inafadhili pia mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 ukutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha nchi za Tanzania na Zambia.

Sambamba kusema kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuiendeleza ajenda ya nishati safi ya kupikia ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab