National News

KEMIKALI YA MAABARA YAUA MWANAFUNZI

Tarehe: 31 May, 2024


#KATAVI:Mwanafunzi Luis Emmanuel (17) aliyekuwa anasoma katika  shule ya Sekondari St. Mary's katika  Manispaa ya Mpanda mkoani    Katavi  amefariki dunia mara baada ya  kunywa kemikali inayodhaniwa kuwa ni Ethanol katika Maabara ya shule hiyo wakiwa na wanafunzi wengine wawili wakifanya usafi katika Maabara hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusiana na tukio hilo wanafunzi hao  ambao walikuwa wanasoma kidato cha nne katika Shule hiyo  walikuwa wakifanya usafi katika maabara ya kujifunzia masomo ya Sayansi kwa vitendo iliyopo shuleni hapo 

Katika usafi huo walikuwa wakisimamiwa na Mwalimu  John Mtafya ambaye alitoka nje kuendelea na shughuli nyingine za kimasomo na  kuwaacha wanafunzi hao wakiendelea na usafi na baadaye walipoingia katika chumba cha kuhifadhia kemikali walichukua kemikali hiyo ya Ethanol na kuinywa na baadaye walipomaliza  kufanya usafi waliendelea na masomo pasipo kusema chochote kuhusu kunywa kemikali hiyo.

Hata hivyo Wanafunzi  wengine wawili Evangelist Deodatus (20) mpaka sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi huku  Anastasia Zakayo (17) hali yake ikiendelea vizuri ambapo  anaendelea na masomo yake.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab