National News

SERIKALI YAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAWEKEZAJI

Tarehe: 30 May, 2024


#BUNGENI:Serikali imesema kuwa imefungua milango pamoja na kutoa fursa kwa wawekezaji wakubwa wa kimkakati wanapata nafasi.

Hayo yamesemwa leo tarehe 30 Mei, 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Bungeni Jijini Dodoma na ambapo pia ametoa wito kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza nchini kwamba serikali inahakikisha kuwa wanapata fursa za kupata punguzo kwenye maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na masharti ya kikodi kupungua.

Aidha ameongeza kuwa fursa nyingine ni kwamba urasimu nao umepungua na kuongeza kuwa ndio sababu Tanzania imeendelea kushuhudia wawekezaji wengi wakiingia nchini. 


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab