Sports

BARRES BADO YUPO SANA MASHUJAA

Tarehe: 30 May, 2024


#MICHEZO: Klabu ya Mashujaa kupitia kwa Mwenyekiti wake imethibitisha kuendelea na kocha wake Abdalah Barres katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. 

Akizungumza na wanahabari mapema leo hii katika Ofisi za Chama cha Soka mkoa wa Kigoma Mwenyekiti wa Mashujaa Meja Abdul Tika, amesema kuwa haoni tatizo kwa Mwalimu Barres bali tatizo lipo kwa wachezaji na wamepanga kuongeza wachezaji katika timu hiyo kupitia kamati ya usajili ya timu hiyo. 

Aidha, kuhusu Jezi za timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao, Meja Tika amesema Jezi zitafika mapema na zitapatikana katika maeneo yote na za kila size. 


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab