SERIKALI INADHAMINI KWA 100% WANAFUNZI WANAOSOMA SAYANSI
Tarehe: 27 May, 2024
#ELIMU:Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali imeanzisha udhamini (Scholarship) maalum kwa wanafunzi wanaofaulu masomo ya sayansi ambapo watasomeshwa na Serikali kwa asilimia 100 kwa gharama zote zikiwemo za kujikimu, chakula, mabweni na vifaa vya elimu hadi mwanafunzi atakapomaliza masomo yake.
Profesa Mkrnda ameyasema hayo jijini Tanga wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayozikutanisha taasisi, mashirika, wadau wa maendeleo, asasi, watunga sera, wabunifu, wagunduzi na wadau wengine kutoka ndani na nje ya nchi, kwa ajili ya mijadala na kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya elimu, ujuzi na ubunifu.
Aidha ameongeza kuwa maadhimisho hayo ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yatafanyika mkoani Tanga kwa miaka mitatu mfululizo ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali katika kuongeza hamasa ya kukuza elimu, ujuzi, na matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo za kusaidia kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii pamoja na kuchagiza maendeleo ya nchi kwa ujumla.