National News

MAKONDA KUWAPIGA SPANA WANAOTETEA UZEMBE

Tarehe: 27 May, 2024


#ARUSHA: Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuwa atawapiga spana wale wote wanaojitokeza kutetea uzembe wa watu ambao wanakwamisha miradi inayotolewa hela na Rais Samia Hassan Suluhu.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo wilayani Monduli mkoani humo ambapo ni mwendelezo wa ziara yake ya siku sita katika halmashauri za Mkoa wa Arusha huku akisema kuwa  kwanini Rais Samia alipotukanwa kupitia mitandao ya kijamii hawajajitokeza watu kukemea leo hii watu wanasema anadhalilisha watu.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab