#HABARI: Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange (Mb) amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya Afya nchini Kote ili kuendelea kuwasaidia na kuwahudumia Wananchi katika maeno mbali mbali
Mhe. Dkt.Dugange amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Jackson Gidion Kiswaga Mbunge wa Jimbo la Kalenga aliyeuliza Je Serikali haioni haja kuunga mkono jitihada za Wananchi wa Kalenga katika ujenzi wa kituo cha Afya cha Kibena.
“kupitia mradi wa usafi wa mazingira serikali ilitoa mil. 74.9 kwaajili ya uboreshaji wa vyoo, mifumo ya maji safi na maji taka Pamoja na ujenzi wa kichomea taka, ambapo maboresho ya miundombinu hiyo imekamilika na inatumika” Dkt. Dugange.