National News

MAREKEBISHO SHERIA 13 KUPUNGUZA KERO KWA WAFANYABIASHARA

Tarehe: 23 May, 2024


#DAR ES SALAAM:Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa amesema kuwa jumla ya sheria 13 zimefanyiwa marekebisho ili kupunguza kero kwa wafanyabiashara hasa maeneo ya mipakani pamoja na kuongeza ushiriki wa wananchi katika kujenga uchumi wa viwanda.

Waziri Majaliwa amebainisha hayo Jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la pili la biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Uganda huku akisema kuwa serikali ina nia njema kwa wawekezaji na wafanyabiashara hivyo haiwezi kuvumili vikwazo vyovyote dhidi yao.

Aidha amebainisha kuwa serikali ya Tanzania imedhamiria kuongeza kipato kwa wananchi kupitia sekta ya biashara na kufikia malengo yake pamoja na kupitia sheria na sera za uwekezaji.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab