National News

"JESHI SIYO SEHEMU YA SIASA,NI SEHEMU MAHSUSI"- TAX

Tarehe: 20 May, 2024


#DODOMA: Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax amesema Migogoro ya ardhi inayohusisha maeneo ya Jeshi inapaswa kutatuliwa kwa mashauriano kwa kufuata Sheria zilizopo na si Kisiasa 

Akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2024/25 amesema maeneo ya Jeshi ni maalum kwa shughuli za Kijeshi ikiwemo Ulinzi wa Taifa na hivyo Viongozi na Wananchi wanatakiwa kuyalinda ili kuepuka Migogoro isiyo ya lazima

Ameongeza "Jeshi si sehemu ya Siasa, ni Taasisi mahsusi kwa kazi mahsusi, naomba tusishawishike sisi kama Viongozi na Wananchi kuchukua hatua zitakazoleta taharuki, chuki na vurugu kati ya Wananchi na Jeshi letu."