National News

UTOVU WA NIDHAMU WAMPONZA ADAM ADAM MASUJAA FC

Tarehe: 20 May, 2024


#MICHEZO: Klabu ya Mashujaa imeachana na aliyekuwa mchezaji wake (mshambuliaji) Adam Adam kwa kile kinachotajwa kama utovu wa Nidhamu.

Akizungumza na Playground ya Main Fm msemaji wa Mashujaa Fc Captain Kimwagu amesema kwa sasa Adam Adam yupo pembeni ya timu kutokana na ishu za utovu wa Nidhamu.

"Ni kweli Adam Adam sasahivi yupo pembeni ya timu kwa maana ya ishu za Utovu wa nidhamu, kama unavyojua timu inaundwa na group haiundwi na mtu mmoja, kwahiyo kwa sasa focus yetu sio Adam Adam lakini habari rasmi kuhusu mchezaji huyo itatoka" Amesema Capt. Kimwagu.

Katika michezo mitatu iliyosalia kwa Mashujaa kukamilisha ratiba ya Ligi kuu, leo itakuwa inatupa karata yake ya kwanza katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons mkoani Mbeya na baada ya hapo watakuja kumaliza michezo miwili katika uwanja wa Nyumbani dhidi Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar.
..........................
Powered by
@nbc_tanzania
@vertexsecuritiestz
@apexattorneysadvocates

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab