National News

NYAMA YA MBUZI YAENDELEA KUWA KINARA MAUZO NJE

Tarehe: 14 May, 2024


#HABARI: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa mauzo ya nyama nje ya nchi yameongezeka kutoka tani 1,774 mwaka 2020/2021 hadi kufikia tani 14,701 mwaka 2022/2023.

Waziri Majaliwa ameyasema kweny hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa Vijana kilichopo Kongwa mkoani Dodoma ambapo kituo hicho
 ambacho ni maalum kwa ajili ya unenepeshaji wa mbuzi kimegharimu sh. bilioni 1.6 na kuongeza kuwa hatua hiyo imechangiwa na ushirikiano wa kibiashara na mataifa mbalimbali duniani uliohamasishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Masoko ya nyama yameendelea kuongezeka na  kuzifikia nchi 12 ambazo ni Bahrain, Comoro, Hong Kong, Jordan, Kenya, Kuwait, Oman, Qatar, Rwanda, Saudi Arabia, UAE na Vietnam.”

Pia ameongeza kuwa nyama ya mbuzi imeendelea kuongoza katika mauzo ya nyama nje ya nchi ambapo imechangia asilimia 70.1 ya mauzo yote na kwamba  inathibitisha kwamba mradi huu ambao wameukabidhi  una manufaa makubwa ya kiuchumi katika nchi kwa kuwa nyama ya mbuzi ina uhitaji mkubwa ndani na nje ya nchi.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa vijana kuitumia fursa ya uwepo wa kituo hicho kwa manufaa yao binafsi na manufaa ya taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo, Abdallah Ulega amesema kuwa sekta ya mifugo inawahitaji sana wadau, wafugaji, wafanyabiashara, walaji na watoa huduma za afya katika kuongeza tija na kuongeza uzalishaji.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab