National News

SERIKALI IMEIMARISHA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI

Tarehe: 13 May, 2024


#BUNGENI:"Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi katika hospitali ngazi ya taifa, kanda, maalum na hospitali za mikoa. Aidha, kutokana na uwekezaji wa kimkakati uliofanywa na Serikali wa kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, huduma mpya 16 za ubingwa bobezi zilianzishwa nchini. Katika kuimarisha na kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na huduma za ubingwa na ubingwa bobezi, wizara inaendelea kutekeleza Mpango kabambe wa kusogeza huduma za kibingwa kupitia huduma za Mkoba (Dkt. Samia Specialized Outreach Program) katika ngazi ya mikoa na halmashauri. Lengo kuu la mpango huu ni kusogeza huduma karibu na wananchi, kupunguza gharama za upatikanaji wa huduma za kibingwa na kujenga uwezo wa wataalamu katika kuendelea kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi"

"Wizara inaeendelea kutekeleza Mpango wa Huduma za Mkoba za Kibingwa katika ngazi ya Halmashauri zote 184 na vituo vya afya 72 ambapo seti ya Madaktari Bingwa wa fani tano (5) wanashiriki katika kila Hospitali ya Halmashauri kutoa huduma za kibingwa na kujenga uwezo wa wataalamu katika ngazi ya Halmashauri. Niwashukuru pia viongozi wote katika ngazi za Mikoa na Halmashauri kwa kuwapokea na kuwawekea wataalamu wetu mazingira mazuri ya kufanya kazi. Nitoe rai kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi pindi huduma hizi zinaposogezwa karibu na maeneo yao. Ninawaahidi kuwa Mpango huu utaendelea mpaka tutakapokamilisha Mikoa yote na Halmashauri zote"-  Ummy Mwalimu

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab