National News

WADAIWA KODI ARDHI WATAKIWA KULIPA NDANI YA SIKU 30

Tarehe: 10 May, 2024


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amewataka wamiliki wa ardhi wanaodaiwa kodi ya  pango la ardhi kulipa kodi husika ndani ya siku 30 kuanzia hii leo Mei 10 2024 kwani kwa kutofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao

Waziri Silaa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Da s Salaam ambapo pia amebainisha kuwa miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa dhidi ya watakao kiuka agizo hilo ni pamoja na kuwafikisha mahakamani na vilevile kubatilisha milki zao

Kadhalika amewataka watumishi wa sekta ya ardhi kuratibu mazingira rafiki ili kutoa fursa kwa wananchi kupata huduma kwa ufanisi huku akibainisha kuwa ofisi za ardhi za mikoa na halmashauri zitakuwa wazi hadi saa mbili usiku kwa siku za kazi

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab