National News

BILIONI 786.7 ZIMETUMIKA KUWAKOPESHA WANAFUNZI ELIMU YA JUU

Tarehe: 07 May, 2024


#BUNGENI: Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda leo, Mei 07, 2024 wakati akiwasilisha Bungeni Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema Serikali imeendelea kuimarisha fursa za upatikanaji wa elimu ya juu kupitia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

“Serikali imetoa mikopo kwa wanafunzi 229,652 (mwaka wa kwanza 83,640 na wanaoendelea 146,012) yenye jumla ya Shilingi bilioni 786,724,730,000.

“Aidha imetoa mikopo kwa wanafunzi 2,299 wa ngazi ya stashahada yenye jumla ya Shilingi bilioni 6,114,790,500.

“Vilevile imekusanya jumla ya Shilingi bilioni 132,731,358,063.47 sawa na asilima 55 ya lengo la kukusanya Shilingi bilioni 241 kutokana na mikopo iliyoiva,” amesema Prof. Mkenda

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab