National News

WANANCHI KUNUFAIKA NA MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA

Tarehe: 19 Apr, 2024


Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Pindi Chana, amemuhakikishia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ya kwamba kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) inawafikia watanzania wote kila kona ya nchi na kuwasaidia katika mambo yote yanayohitaji msaada wa kisheria na kumwambia kuwa kampeni hiyo imesaidia kungeza uelewa kwa watanzania wengi na kuona umuhimu wa kuzingatia na kufuata sheria na taratibu za nchi.

Akizungumza mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya stendi za zamani ya Makambako mkoani Njombe katika muendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu, Balozi Pindi Chana ameitambulisha kwa Katibu Mkuu na Wananchi wote timu ya kikosi kazi maalum inayozunguka katika kutoa msaada huo wa kisheria kama ilivyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"qHatulali tupo mtaa kwa mtaa, tunafika nyumba kwa nyumba mpaka kieleweke kuhakikisha watanzania wanapatiwa msaada wa kisheria na ndio kazi tuliyotumwa na Rais wetu kwa mapenzi yake ya dhati kwa Watanzania wote" Alisema Balozi Dkt. Pindi Chana.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab