National News

BIL. 322 KUTUMIKA UJENZI MELI MPYA KIGOMA

Tarehe: 16 Apr, 2024


#Habari: MKUU wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kali ameeleza miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita huku akimshukuru Rais Dr.  Samia Suluhu Hassani kwa namna ambavyo amewezesha fedha za miradi katika Wilaya hiyo.   Pongezi na Shukrani hizo amezitoa leo April 15, 2024 katika Kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kilichofanyikia katika Ukumbi wa Kanisa la Angrikani uliopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji. 

Kikao kazi hicho kimehusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Waratibu elimu Kata,  Wakuu wa Shule, Wenyeviti wa Mitaa,Vijiji na Vitongoji kutoka Halmashauri zote mbili  Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. 

Katika Kikao kazi hicho amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassani imeitendea haki Mkoa na Wilaya za Kigoma, ambapo katika Wilaya hiyo imetekeleza na inandelea kutekeleza Ujenzi wa Meli Mpya Mkoani Kigoma kwa gharama Tsh Billion 322/=, Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Uhasibu (TIA) unaoendelea kwa gharama ya Tsh Billion 37/=, na Ujenzi wa Bandari ya Kibirizi na Ujiji  kwa gharama ya Tsh Billion 37/=. 

Miradi mingine aliyoitaja ni pamoja na Ujenzi wa Reli ya Kisasa(SGR) kipande kutoka Kigoma hadi Tabora kwa gharama ya Tsh Trioni 6/=, Ujenzi wa Hospitali mbili (02) unaoendelea Manispaa ya Kigoma Ujiji naHalmashauri ya Wilaya ya Kigoma. 

Miradi mingine ni ya kupitia mradi wa TACTICS ambayo ni pamoja na Ujenzi wa Barabara ya Wafipa-Kagera yenye urefu wa Km 2.434, Daraja la Mto Ruiche, Ujenzi wa barabara ya Bangwe-Burega- Ujiji yenye urefu wa Km 7.1, Ujenzi wa mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua katika maeneo ya Bangwe,  Burega,  Rutale,  Mlole , Bushabani, Mji mwema,  na Katonyanga yenye urefu Km 5.288, Ujenzi wa Kisasa soko  la Mwanga, Ujenzi wa Kisasa wa Soko la mazao ya Uvuvi Katonga, na Ujenzi wa barabara ya Old Kasulu yenye urefu wa Km 7. 

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab