National News

VIJIJI VYOTE 4071 KUUNGANISHIWA UMEME KABLA YA MWEZI WA SITA

Tarehe: 15 Apr, 2024


#REA: MKURUGENZI Mkuu wa wakala wa Nishati vijijini REA  Mhandisi Hassan Saidy amesema kabla ya kufika mwezi wa sita mwaka huu watahakikisha vijiji  vyote 4071,nchini vitakuwa vimepata umeme.

Mhandisi Saidy ameyasema hayo   wakati wa ugawaji wa tuzo kwa mwaka 2024 kwa wakandarasi waliofanya vizuri na kumaliza miradi  kwa wakati.  

Vilevile amesema kwa sasa mkandarasi ambaye hatafanya kazi kwa wakati hatopata mkataba  mwingine na kwamba  vyeti hivyo kwa  wakandarasi vimetolewa ili waweze kupata motisha ya kufanya kazi kwa bidii.

Kwa upande wake mkurugenzi wa TANESCO kanda ya Mashariki mhandisi Kenneth Boymanda amesema wanaamini tuzo hizo zitawasukuma wakandarasi wasiofanya vizuri kwenye miradi yao kuhamasika  katika kujituma na kuomgeza weledi huku mshindi wa kwanza wa wa tuzo hiyo  Mhandisi Shaban Zacharia kati ya watano waliomaliza kazi kwa 2024 akisema kuwa tuzo hiyo ni chachu kwao na kuahidi kujituma na kusimamia ipasavyo miradi wanayopewa.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab